Sitosema kuhusu elfu moja Kenda kenda na Saba. Mtasema eti sikua hata miaka Saba. Hata sitogusia ya Saba saba. Wacha nseme kuhusu elfu mbili na saba. Hapo nlikua na saba mara mbili. Niliona, nakumbuka na nita nena. Mkazozana ndume wawili muongoze. Nyasi sisi ole wetu.. Tukaumia. Tukauana zaidi ya elfu saba
Damu ilipomwagwa😢, mkaelewana. ☺Makovu zaidi ya saba mtu mmoja. Makaburi zaidi ya saba boma moja. Mkatupa jina I. D. P mkatupa ahadi Za mashamba. Mashamba yaliyokua yetu.. Na sitosema. Majeraha yapo mpaka sasa
Miaka saba iliyopita, Katiba ni kongwe mkasema. Mkatugawa tena.. eti chungwa na ndizi. Hatima ikawa. Mkapata viti vingi. Kukawa nchi ndogo arubaini na saba. Vya kina mama pia eti jinsia sawia. Miaka saba hii… Nyasi tumekipata. Ushuru tumelipa mpate mishahara ya Miraba
Sasa tunakufa njaa. Janga alilopigana nalo baba wakwanza wa taifa. Masanduku ya chakula nadhani mazito Mazito kuliko yale ya kura mkitafuta viti. Lakini si neno.. tunangoja mtupe pay bill. Tufanye michango…. Kenyans for kenya Na tutafanya…. Tupate milioni saba
Juzi nkaskia zatafutwa milioni… Samahani bilioni ishirini na moja. Kumbe tuko karne ya ishirini na moja. Tena ati sio nyingi ni milioni.. Oo bilioni saba.. Mnisamehe nkikosa.. Pesa kama hizo sijaona wala kushika. Hizo hazingetosha chakula cha mkenya? Hata wangetupa kila mmoja milioni… sarafu Si haba zingebaki.
Lakini sio neno… Nadhani hata jua.. Limejua. Limeghadhabika na lina makali Miaka saba yote hii.. Natumai hatutofikisha sabini na shida zote hizi.
#hadithinisemazo Nyamburandungu. Mach 18-2019
Weh! Kali hiyo…karibu nijiume ulimu wangu huu lakini kwa kweli hapo naye umeweza!
I like the way your work mirrors our society